Friday, November 9, 2012

WALTER CHILAMBO AJINYAKULIA MILIONI 50 KUTOKA EBSS

Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar)

WALTER CHILAMBO ndiye mshindi wa Shindano la Epic Bongo Star Search (EBSS)  2012. Kufuatia matokeo hayo Kalambo amejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania kutoka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel.

Chilambo ametwaa ubingwa huo baada ya kumwangusha mwana dada kutoka Zanzibar ambaye alikuwa ni mshindani wake wa karibu katika kinyang’anyoro hicho Salma Yusufu.

Washiriki wa Washindano la EBSS 2012 ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa kuanza kwa fainali hizo. Ni ndani ya Ukumbi wa Diamond Jijini Dar es Salaam. Mshindi kuondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania.

No comments:

Post a Comment