Leo Mkutano
uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kudhibiti ukimwi uliofanywa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania umefanyika jijini Dar es Salaam
katika hoteli ya Blue pearl.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dr Fatma H. Mrisho amesema
kuwa katika kuhakikisha kuwa
wanadhibiti ukimwi Tanzania bado wamekuwa wanakumbana na Changamoto mbalimbali
ikiwemo ya wanaume kutokwenda kuynunua Madawa ya kupunguza makali ya Virusi vya
Ukimwi ARV na badala yake wanawatuma wanawake.
Amesema kuwa, wamegundua hivyo baada ya kuona kuwa wanawake ndio wanaokwenda kuchukua
dawa hizo peke yao na mara kwa mara hata kabla siku za kumeza dawa
hazijakwisha.
Ameongeza kuwa vijana wengi hawataki kwenda kupima na badala
yake wanaenda kupima wakati mwili umeshadhoofika jambo linalowapelekea
kuchelewa kupatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi.
Bi Fatma amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwenda
kupima Afya zao ili waweze kujua kwamba wameambukizwa au lah na
kuongeza kuwa kufanya hivyo kutawasaidia wao kufikia malengo ya kutokomeza
kabisa Ugonjwa wa ukimwi nchini.
|