Waziri wa Maji Prof
Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili unaoendelea katika Ukumbi wa mikutano Bluer
Pearl jijini Dar es Salaam ambapo Warsha hiyo imewakutanisha wadau wa sekta ya maji.
Prof Maghembe amesema kuwa
wanampango wa kuhakikisha kuwa katika kipindi cha malengo ya milenia
mpaka kufikia mwaka 2015 asilimia 90 mpaka 98 ya wakazi wanaoishi mijini
wanapata maji safi na salama.
Ameongeza kuwa malengo
ya milenia ni kuhakikisha kuwa asilimia 65 ya wakazi wa vijijini wanapata maji ambapo
mpaka sasahivi kwa vijijini tayari wamefikia 58% jambo ambalo
wanategemea kuhakikisha kuwa
kufikia mwaka 2015 wawe wamefikia malengo hayo.
|