Friday, November 16, 2012

SHULE YAFUNGWA KUTOKANA NS VURUGU ZA KIDINI WAISLAMU WAWATUHUMU WAKRISTO KUINGIA NA KITIMOTO SHULENI

Taarifa zilizopatikana muda na Zisizo rasmi ni kwamba shule ya Sekondari Kibiti imefungwa baada ya vurugu kubwa kutokea kati ya wanafunzi wa Kikiristo na Waislam.

Taarifa hizo zinasema kuwa, wanafunzi wa kikiristo wamekuwa wakiwatuhumu wenzao kupiga kelele na kushindwa kusoma wakati waislamu wamekuwa wanawatuhumu wakiristo kuwa wana kwenda kununua KITIMOTO(nyama ya Nguruwe) na kuingia nacho katika mazingira ya shule.

Baada ya vurugu hizo Mkuu wa shule ameamua kufunga Shule hiyo bila kutoa lini itafunguliwa.



MAASINDA itazidi kuwaletea Taarifa kuhusiana na Sakata hili.

No comments:

Post a Comment