Kama msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika
kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa Tunzo nyingi zaidi akiwa na
albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee
ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta
kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo
cha TV cha EATV
Jaydee amesema kuwa kipindi hicho kitakuwa kinaelezea maisha yake halisi kuanzia alipotokea mpaka alipo sasa ambapo amesema kuwa kipindi hicho kitaanza kurushwa Jumapili saa tatu usiku na itakuwa ni kila jumapili muda kama huo huo.
Amewataka Watanzania kufwatilia kipindi hicho ili waone Mafanikio yake na wao waweze kuiga na kufwata Ndoto zao.
Judith Wambura akifafanua Jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) na anayeonekana kushoto kwake ni Mkuu wa Vipindi vya Kwenye Televisheni EATV Bi, Lyidia Igarabuza |
Hapa wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari |
No comments:
Post a Comment