Waziri wa Uchukuzi Dk Harrisn Mwakyembe |
WAZIRI wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe ameifuta Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), na kuteua wajumbe wengine wanane watakaounda Bodi hiyo kuanzia juzi Navemba 6 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Mwakyembe iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam
jana, alichukua uamuzi huo kutoakana na mamlaka aliyonayo chini ya
Kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Bandari na Kifungu cha 1(2)(i) cha Sheria
ya Bandari ya mwaka 2004.
Tarifa hiyo iliwataja wajumbe wa
Bodi iliyovunjwa kuwa ni pamoja na Dunstan Mrutu, Injinia George Alliy,
Alh. Mtutura Mtutura, Emmanuel Mallya, Mwantum Malale na Maria Kejo.
Ikifafanua zaidi taarifa hiyo,
ilisema kwa bahati mbaya wajumbe wawili wa Bodi hiyo iliyofutwa
wamefariki dunia bila kuwataja majina hivi karibuni.
Wajumbe waliyoteuliwa kuingia
kwenye Bodi hiyo mpya kuwa ni pamoja na Dk Jabiri Bakari, John Ulanga,
Caroline Temu, Jaffer Machano, Dk Hizldebrand Shayo, Saidi Sauko,
Injinia Julius Mamiro na Asha Nassoro.
Taarifa hiyo ilieza kuwa
mabadiliko hayo ni sehemu tu ya hatua ambazo Wizara inachukua kurejesha
ufanisi katika Mamlaka hiyo ili iweze kuchangia zaidi kwenye pato la
Taifa.
Waziri aliagiza menejimenti ya
TPA kuwapa nyaraka zote muhimu Wajumbe wapya wa Bodi ili waweze
kujiandaa kabla hajakutana nao ndani ya siku kumi kuanzia juzi ili
kuingia nao Mkataba wa ufanisi.
No comments:
Post a Comment