JUKWAA LA KATIBA TANZANIA bado tumebaini mapungufu kadhaa katika
mchakato wenyewe wa ukusanyaji maoni kwa mwezi huo, ikiwa ni pamoja na Tume
kuendelea kutumia huduma ya wataalam wa lugha za alama ili kusaidia watu wenye
ulemavu wa kusikia na kuzungumza.
Mikutano kuendelea kufanyika asubuhi na mchana na hivyo kuwanyima fursa
ya ushiriki wananchi wengi hususani wanawake.na kucheleweshwa kwa utoaji wa
ratiba na hivyo kufanya maandalizi yawe duni katika maeneo wanakojiandaa kwenda.
Kwa ujumla, Tume imeshindwa kushughulikia baadhi ya mapungufu ya
Mchakato wa ukusanyaji wa maoni kwa sababu ya kutaka kuwahi kukamilisha
mchakato katika tarehe iliyopangwa bila kuzingatia haja ya watanzania wote
kutoa maoni yao bila vikwazo.
Inasikitisha kuwa hata ratiba ya mzunguko wa mwisho wa awamu ya kwanza
utakaohusisha ukusanyaji maoni katika mikoa ya Dar es Salaam, Mara, Simiyu, Geita,
Arusha na Kusini Magharibi ilikuwa haijatoka na kusambazwa hadi Alhamis wiki
hii. Ukusanyaji maoni katika Mikoa hiyo unaanza Jumatatu tarehe 19 Novemba na
utaendelea hadi 12 December 2012.
No comments:
Post a Comment