Saturday, November 17, 2012

PAMOJA SANAA GROUP WAONYESHA MFANO KWA WASANII WENGINE: WATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

Kikundi cha sanaa cha Pamoja Group kikijiandaa kuingia ndani kwenye Nyumba ya kulelea Watoto yatima kwa ajili ya kutoa msaada.
 
Kikundi cha Sanaa cha  Pamoja kimetoa Msaada kwa Watoto yatima  cha CHAKUWAMA  kilichopo jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na waandishi wa Habari leo wakati wakitoa Misaada hiyo wasanii hao wamesema kuwa wameguswa na wakaona watumie kile kitu kidogo wanachokipata kugawana na wengine wenye maisha magumu.

Wasanii wa Pamoja Group wakishangilia kuwaona watoto hao


Mlezi wa Kundi la Pamoja Sanaa Group akimkabidhi motto Yatima Hadija Joseph,  Juice ikiwa ni moja ya Baadhi ya Bidhaa walizowapa watoto hao.

Mafuta nayo yalikuwepo katika baadhi ya Msaada walioutoa

Maji pia

Kikundi kiliamua watoto hao waonje juice hapo hapo wakiwa wanaona

Watoto wanafurahia zawadi kutoka kwa Pamoja Sanaa Group


Kassim Obedi Mwenyekiti wa Kikundi hicho,akizungumza na waandishi wa habari  ambapo amesema kuwa  wametumia kiasi cha Shilingi laki tatu kutoka katika mifuko yao wenyewe kuweza kununua baadhi ya  vyakula na vinywaji kwa ajaili ya watoto hao.Aidha amewaomba mashirika Binafsi kuwasaidia Kikundi hicho kwa kuwadhamini ili waweze kuendelea kusaidia jamii.

Tupo pamoja Hoeme Boy

No comments:

Post a Comment