Wednesday, October 10, 2012

ZUKU SASA KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

Irene Muratha Mkuu wa Masoko ya Wananchi Satellite na Fadhili Mwasyeba Meneja Wanachi Satellite Tanzania akizungumza na mwandishi wa habari (wasio katika picha) wakati wa uzinduzi wa programau ya kuwazawadia weteja  Zuku Tunakuthamini  - Pata TV Bure . Programu hii itawazawadia wateja ambao wataunganisha wateja wapya kwa mtandao wa Zuku. Hapo nao pia ni Veranda Raphael Msaidizi wa Zuku

Veranda Raphael Meneja msaidizi masoko Zuku, akielezea wandishi wa habari (wasio katika picha) wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwazawadia wateja ya Tunakuthamini Zuku - Pata TV Bure Programu hii itawazawadia wateja ambao wataunganisha wateja wapya kwa mtandao wa Zuku. Hapo naye ni ni Irene Muratha, Mkuu wa Masoko  Wananchi Satellite na Fadhili Mwasyeba  Meneja Wananchi SaelliteTanzania.

Fadhili Mwasyeba  Meneja Wananchi Satellite Tanzania (katikati) akielezea wandishi wa habari kuhusu mtandao wa mawakala wa Zuku wakati wa uzinduzi wa programu ya kuzawadia wateja ya Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure. Programu hii itawazawadia wateja ambao wataunganisha wateja wapya kwa mtandao wa Zuku..Sambamba ni Irene Muratha Mkuu wa Masoko Satellite Wananchi na Veranda Raphael wa Zuku
Zuku inayomilikiwa na kampuni ya Wananchi, imezindua programu ya kuwazawadia wateja wao ya  Zuku Tunakuthamini – Pata TV Bure hapa jijini Dar es Salaam. Zuku Satellite Pay TV ni kingamuzi cha burundani cha televisheni ambacho kinachanneli zaidi ya 70.

Akizungumza na waandishi wa habari, Irene Muratha Mkuu wa Masoko ya Wananchi Satellite alibainisha kuwa Tanzania ni moja ya uchumi kukua kwa kasi katika Afrika Mashariki na kampuni ya Wananchi Group - kampuni inayomiliki Zuku Satellite Pay TV- ni miongoni mwa wawekezaji katika nchi. Aliongeza kuwa, "Tangu uzinduzi wa Zuku Satellite Pay TV mapema kwa mwaka, tunaendelea kuwekeza nchini na na udhamini wetu wa ZIFF ambayo inaweka filamu za tanzania kwenye jukwaa la kimataifa, Hyped East Afrika na leo hivi na leo tunazindua uwekezaji wetu mpya wa programu ya Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure.

Programu hii ya kuwazawadia wateja, itahitaji wateja kuungananisha wateja  kumi (10) au kuunganisha wateja watano (5) wateja wapya na kupatat uhakika wa kushinda televisheni ya inchi 42 na inchi 22. Programu hii ni ya kipekee kwa kuwa wateja wote ambao watakaohudhuria wanauhakika wa kushinda tena na tena. Programu hii itaendelea hadi Desemba 31, 2012.

Veranda Raphael, Msaidizi Masoko Zuku Tanzania, alielezea kuwa programu hii ni kwa wateja waliopo na wateja wapya ambao watakaoshiriki. Maelezo ya vigezo na masharti zinapatikana kwa wakala wote wa Zuku nchini

Zuku TV inatoa uchaguzi mpana wa burudani,  habari, michezo, sinema, na dini na muziki. Zuku pia inamiliki channeli kam vile Zuku Afrika, Zuku Movies, Zuku Sports na Zuku Action. Kingamuzi cah Zuku kinatpatikana kote nchini katika mawakala wake and kujiunga ni Ths 92,000.