Monday, October 15, 2012

ZANZIBAR:WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WATOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliotishwa na Tume hiyo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kutoka kulia ni Wajumbe  wa Tume hiyo,  Profesa Paramagamba Kabudi, Suleiman Ali, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali, Mjumbe wa Tume Joseph Butiku, Katibu wa Tume Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Asha Bakari Makame akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk, akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jussa Ladhu akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar , ambapo wajumbe hao walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.


Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha , akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe wa Baraza hilo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na Mjumbe wa Tume Joseph Butiku.