Monday, October 15, 2012

KUJIKOMBOA KWENYE UMASKINI NA KUMILIKI RASLIMALI ZETU WENYEWE HAPA KWETU TANZANIA KWA HALI HII ITAWEZEKANA?

Mkuu wa Wilaya ya Muheza Subira Mgalu
ZAIDI ya watu wazima 11,241  katika wilaya ya Muheza mkoni Tanga hawajui kusoma,kuhesabu na kundika imefahamika.
 Hayo yalisemwa na Afisa Elimu ya Watu wazima wilayani Muheza, George Lukoa wakati sherehe za maadhimisho ya Siku ya kilele cha elimu ya watu wazima iliyofanyika katika kijiji cha Bwitini.
Akizungumza na Fullshangweblog.com, Lukoa, alisema kuwa kati ya hao wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu, wanaume ni kati ya  4,407 huku wanawake  wakiwa 6,834 sawa na asilimia 12.08.
 Aidha, kata ya Mhamba kuna jumla ya watu hao 307 wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ambapo idadi yao, wanaume ni 93, wanawake 214 sawa  na asilimia 32.11 hiyo, ni kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2011.
 Lukoa alisema kutokana na  hali hiyo ni vema uongozi wa wilaya kwa kushirikiana na kata pamoja na vijiji kuja na mikakati mipya itakayosaidia kupunguza idadi ya watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu wilayani hapa
 Naye  mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Mgalu, alitoa wito kuwa kamati za elimu ya watu wazima ngazi ya vijiji, mitaa na kata zifufuliwe ili ziweze kurahisisha ufuatiliaji wa suala zima la maendeleo yote ndani ya wilaya hiyo.

 Mgalu aliwakumbusha wazazi ambao watoto wao hawakubahatika kujiunga na masomo
kupitia mfumo rasmi wa elimu ya msingi wajiunge na MEMKWA ili wajipatie elimu kwa njia hiyo.
Pia alisema kuwa wale ambao hawakupata fursa ya elimu ya sekondari ni vema wakajiunga na mpango wa elimu ya sekondari MESKWA kwa mwaka 2013.
 Mgalu alimalizia kwa kuwaasa wazazi kuwahamasisha vijana katika suala zima la kujiunga na mafunzo mbalimbali katika vituo vya ufundi stadi VETA ili elimu watakayoipata iwasaidie katika kujikomboa kutoka dimbwi la umasikini.