Monday, October 15, 2012

WEMA SEPETU PAMOJA NA AUNT EZEKIEL WAOMBA RADHI KWA KUCHEZA NUSU UCHI WAKATI WA FIESTER WAAHIDI KUBADILIKA

Msanii wa filamu Tanzania Aunt Ezekiel Kushoto akionea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati akiomba radhi kwa Umma kutokana na Kitendo walichokifanya wakati wa Fiester, Wakati wa Fiester Aunt Ezekiel pamoja na Mwenzie Wema walichza Stejini huku wakionyesha sehemu za miili yao ikiwa wazi, Ezekiel amesema kuwa anaomba radhi na anawaahidi watanzania kutorudia kitendo kama hicho kwani amegundua kuwa ni kitendo ch Udhalilishaji.
Wema naye akionyesha ishara ya kuomba radhi kutokana na Kitendo hicho, na alijitetea kuwa alifanya vile kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kucheza jukwaani,"Jukwaa la Fiester lilikuwa ni refu sana na waandishi siku zote wanakaaga kwa chini hivyo ni lazima wangeona kila kitu, hata hivyo napenda kuwahakikishia watanzania kuwa sintorudia na tokea siku ile nimekuwa navaa nguo ndefu kama Jeans ambazo zinasitiri mwili wangu", alisema Wema. Wakati wa kuongea na waandishi wa habari Wema pamoja na Mwenzie walivaa nguo ambazo ni Ndefu za kuwapendeza na ambazo zinasitiri miili yao swali ni Je, Wasanii hawa watabadilika kama walivyo ahidi kubadilika  mbele ya Umma?


Aunt Ezekiel kushoto na Wema walivaa hivi jana wakati wakiongea na waandishi wa habari
Huyu ni Aunt Ezekiel akiwa jukwaani wakati wa Fiesta na hii ni picha moja wapo iliyomfanya aombe radhi

Aunt Ezekiel

Huyu naye ni Wema Sepetu wakati wa Fiesta akionyesha nusu Uchi kwa Watazamaji