Monday, October 15, 2012

MALAWI WAMFIKISHA MAHAKAMANI MWANDISHI ALIYEDANGANYA KUFUKUZWA KWA ALOZI WA TANZANIA

Hivi karibuni zilizuka story kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi amepewa saa 48 awe ameondoka nchini humo lakini imebainika kuwa habari hizo ni za uzushi mtupu na kufwatia uzushi huo Seikali ya malawi imemkamata mwandishi wa habari hiyo kutoka  Malawi Justice Mponda(pichani) na amefikishwa mahakamani kwa kufungua "kiwanda cha kutunga uongo" kuwa Serikali ya Malawi imemwamuru Balozi wa Tanzania nchini Malawi kuondoka nchini humo ndani ya masaa 48.

Inasemekana mwandishi huyo alikamatwa nyumbani kwake na polisi wenye silaha mida saa kumi leo alfajiri na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha Blantyre kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani.

Habari kwa hisani ya Mtandao