Monday, October 15, 2012

DK NDUGULILE ABAINI MAKANISA KUMI KUHARIBIWA KATIKA VURUMASHI ZILIZOTOKEA MBAGALA TOFAUTI NA INAVYOTANGAZWA KUWA NI MAKANISA SABA TUU.

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugulile akisalimiana na  Makamu Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies Of  Gog  Askofu Magnus Muiche  wakati alipokwenda kutembelea  pamoja na kutoa pole kwa Makanisa yaliyoharibiwa na Mgogoro wa Kidini ambapo Mbunge alibaini Makanisa kumi yaliyoharibiwa na Sakata hilo ambapo aliweza kutembelea makanisa yote kumi.
 Mbunge wa Jimbo la Kigamboni jana amefanya ziara katika Makanisa yaliyoharibiwa katika Vurumashi zilizosababishwa na Mtoto aliyekojolea Msaafu na kubaini kuwa Makanisa yaliyoharibiwa ni kumi na sio saba kama inavyotangazwa na vyombo vya habari.

Katika Ziara Hiyo Mh Mbunge alifanikiwa kutembelea Makanisa yote yaliyoharibiwa pamoja na kutoa pole kwa Waathirika na kuwataka wawe wavumilivu wakati Dola inafnya kazi yake.

Makamu Askofu wa Kanisa la TAG ambaye kanisa lake lilikumbwa na Vurumashi hiyo alisema kuwa watu walioingia kufanya uharibifu walikuwa wanaharibu pamoja na kupora vitu vingine.
Alisema kuwa katika kanisa lake walikuwa wanavunja vioo vya magari pamoja na Kuchoma Magari lakini kabla ya Kuchoma walikuwa wanaiba baadhi ya vifaa vikiwemo Radio za Magari.
Mh Mbunge (kulia) akiangalia gari liliochomwa katika hekaheka hizo

Kinanda cha Kanisa la KKT kilichoharibiwa na wahalifu hao

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili  Kilutheri Tanzania KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani Mtaa wa Mbagala  Mch, Frank Kimambo akimwenyesha Mh Mbunge baadhi ya Sehemu iliyoharibiwa katika Kanisa hilo ambapo alisema kuwa Ofisi yake ilichomewa kila kiti na hawakuweza kuokoa kitu chochote, na kuongeza kuwa sehemu nyingine iliyoharibiwa ni Madhabau.

Mchungaji wa Kanisa la Agape naye akionyesha sehemu ya Iliyoharibiwa katika Kanisa lake ambapo alimtaka Mbunge kuitaarifu serikali kuwa Makanisa yaliyoharibiwa ni kumi na siyo saba kama inavyo daiwa. na aliongeza kuwa hawataki kusikia Serikali ikisema kuwa waliofanya uhalifu huo ni kikundi cha kihuni, aliitaka Serikali kutamka waziwazi kuwa waliofanya vile ni waislamu.