Friday, October 12, 2012

WAISLAMU WARINDIMA KITUO CHA POLISI MBAGALA WAKIKITAKA KITUO HICHO KIMTOE KIJANA ALIYEKOJOLEA MSAAFU

 Mabomu ya  Machozi yanarindima hivi punde huko mbagala wilayani Temeke  ili kuwasambaratisha waislamu waliondamana  na kukizunguka kituo cha Polisi Kizuiani  wakitaka  Polisi imuachie Kijana wa Mkristo wa Kidato cha kwanza aliyekojolea kitabu cha Dini  ya kiislamu  maarufu kama Msaafu

Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba  kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi ameamua kufanya hivyo baada ya  kutokea Mabishano  kati  ya yeye na Mwenzie kuwa ukikojolea kitabu hicho utakuwa mwendawazimu ambapo kijana huyo mkristo alipinga  na kuamua na kuamua kukojolea Msaafu.


Kijana huyo alikojolea Msaafu ili ahakikishe kuwa kweli atakuwa Mwenda wazimu ama tofauti na baada ya kijana huyo kukojolea kitabu hicho Tukufu ndipo Mwislamu huyo akaamua kuwataarifu waislamu wenzake juu ya Kitendo alichokifanya Mwenzake.
Na mpaka hivi sasa Polisi wameamua kupiga Mabomu ya Machozi ili kuwatawanyisha Waislamu waliokusanyika mahali hapo, ambapo waislamu wengine wanasikika wakisema kuwa ni bora wafie hapo lakini kuondoka hawaondoki.