SERIKALI kupitia wataalamu wake wa kilimo imeanza mkakati
wa kutoa elimu ya kisayansi juu ya matumizi ya mbegu za kisasa na madawa kwa
wakulima ili kukabiliana na uchakachuaji wa mbegu na madawa unaofanywa na
wafanyabiashara wenye tamaa ya
kujiongezea kipato kwa njia ya udanganyifu.
Kauri hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na naibu waziri
wa kilimo,Adamu Malima wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa mbegu,wakulima,na
mawakala wa mbegu kutoka nchini mbalimbali za Afrika uliofanyika jijini Arusha.
Aidha alisema matumizi ya mbegu za mahindi zisizobora
yanaifanya Tanzania kupunguza uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana ukosefu wa
mvua za kutosha ,ambapo kwa sasa Tanzania inazalisha tani milioni 5 za
mahindi pekee huku nchi jirani zikitegemea kununua mazao hapa nchini.
Alisema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya
ukosefu wa mbegu bora zinazoweza kustahimili ukame na kwendana na mabadiliko ya
hali ya hewa ,kwani mbegu nyingi zinazotumiwa na wakulima hapa nchini hazina
ubora na mara nyingi zinachakachuliwan na mawakala wa mbengu .
‘’tayari mkaguzi wa mbegu ameshaanza kazi ya kupitia
upya mawakala wa mbegu na anakwenda vizuri kwahiyo suala la uchakachuaji karibu
linafika mwisho’’alisema Malima
Malima alisisitiza kuwa mkakati wa serikali hivi sasa ni
kusambaza elimu juu ya matumizi ya sayansi kwenye kuboresha mbegu pamoja na matumizi
ya mbolea za kisasa zitakazomwezesha mkulima kuzalisha kiasi kikubwa cha mazao kwa
hekari kidogo.
Alisema kuwa wataalamu wetu hapa nchini hawatumiki kama
inavyokusudiwa badala yake wamekuwa wakitumiwa na nchi zinazotuzunguka kwa
kutoa elimu na kueleza kwamba serikali
imejidhatiti kuhakikisha kuwa wataalamu wake wanasambaza elimu kwa umma ya
matumizi ya mbegu bora kama ngano mahindi ,ngano viazi ,mihogo .
Awali mkurugenzi mtendaji wa sekretalieti ya makampuni
ya mbegu hapa nchini (TASTA),Bob Shuma alisema
kuwa katika jitihada za kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha na
wakulima wanapata ufanisi wa mbegu
zinazostahimili ukame umeanza.
Alisema lengo la mkutano huo ni kugundua mazao
yanayoweza kustahimili ukame na magonjwa ,kubadilishana uzoefu na utekelezaji wa utafiti wa mbegu mpya
zitakazistahilimi ukame ambao tayari
zimeanza kufanyiwa majaribio mkoani Dodoma.
Alisema Mbegu zilizoanza kufanyiwa utekelezaji wa
majaribio hapa nchini,chini ya mpango wa mradi wa wema ni mahindi na pamba.