JUMLA ya wanafunzi 481,414 kidato cha nne leo wameanza
mitihani ya kukamilisha elimu ya kidato hicho huku wakijiandaa kuingia
kidato cha tano , mtihani ambao utakamilika Oktoba 25 mwaka huu.
|
Mtihani huo wa kidato cha nne
ambao una umuhimu kwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla, kwani hutumika
katika uchaguzi wa watahiniwa wanaotarajiwa kujuiunga na masomo ya
kidato cha tano na vyuo mbalimbali.
Aidha, ili watahiniwam na soko
la ajira katika taasisis za umma au sekta binafsi ni lazima mhusika awe
nacheti cha kidato cha nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
na Tanzania Daima, baadhi ya wanafunzi walisema wanatarajia kufanya
mitihani yao kwa mafanikio kwa kuwa wamejiandaa vizuri.
Mmoja wa watahiniwa hao,Sharifa
Haroun alisema anamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na kuwa
makini katika kipindi chote cha miaka minne ya mafunzo.
Naye Mwantumu Nassoro ambaye ni
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mloganzila, wilayani Kisarawe mkoa wa
Pwani, alisema walimu wamejitahidi hivyo kilichobaki ni kukamilsha kazi
iliyoko mbele yao.
Ni hivi karibuni Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kuhusu usalama wa
mitihani, hadi mwishoni mwa wiki mitihani yote ilikuwa salaam, na hakuna
mtihani wowote uliyokuwa umevuja katika ngazi yoyote kuanzia Baraza la
Mitihani, Mikoa na Halmashauri.
Mulugo aliwakumbusha watahiniwa kuwa, kila mmoja wao anapaswa kufanya mitihani hiyo kwa kujitegemea bila kutumia udanganyifu.
Alitoa onyo kwa wale wote watakaobainika kushiriki katika udanganyifu watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Mulugo alitoa witoa wito kuwa
walimu, wasimamizi wa mitihani, wakuu wa shule, viongozi wote, na jamii
kutoa ushirikiano na kuhakikisha kuwa mitihani inafanyika katika
mazingira yenye usalaama na amani.
“Ninaomba wote tuungane kuwaombea watahiniwa wetu baraka za mwenyezi mungu na mafanikio katika mitihani yao”alisema Mulugo.
Akikumbushia walimu
waliyojihusisha na vitendo udanganyifu katika mtihani wa mwaka jana,
alisema walimu hao walipewa adhabu mbalimbali ikiwemo onyo, karipiokali,
kuvuliwa madaraka wakuu wa shule na wengine kushitakiwa TSD.
Aidha, wenye shule binafsi
waliothibitika kusababisha udanganyifu wameandikiwa barua ya kusudio la
kuzuia kudahili wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa muda wa mwaka mmoja.
Imeandikwa na bukuku blog