Friday, October 26, 2012

WAANDISHI WAUKACHA MKUTANO WA WIZARA YA UCHUKUZI

Wizara ya uchukuzi leo imejikuta katika hali ambayo siyo nzuri baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari ambao uliitishwa na Naibu waziri na hatimaye Naibu waziri kushindwa kufika katika mkutano kwa wakati, jambo lililowapelekea waandishi kuondoka kwa kile walichodai kuwa ni  kupotezewa muda wao.
Baadhi ya waandishi wamekaririwa wakisema kuwa imekuwa ni mazoea kwa wizara hiyo kuwadharau waandishi kwani kila wakiita mkutano na waandishi wa habari viongozi wanachelewa kufika  kwa wakati, leo mkutano ulikuwa uanze saa sita kamili mchana kama afisa habari wa wizara hiyo Bw, Biseko alivyowasiliana na waandishi wa habari lakini cha kushangaza ni kwamba waandishi wamefika wizarani kabla ya saa sita kamili lakini wamekaa takriban nusu saa nzima  bila kiongozi yeyote kuja kuzungumza.

Baada ya hapo waandishi waliamua kuondoka kwenda kuendelea na shughuli nyingine na hata baada ya Afisa habari kuagwa alijibu sawa sawa.

Tukio hilo limetokea muda huu katika Wizara ya Uchukuzi jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano katika wizara ya Uchukuzi

Hapa wanaondoka

Wanatoka Ukumbini