Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akisisitiza jambo mbele ya waaandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kikao chake na waaandashi wa habari leo katika makao makuu ya ofisi hiyo. |
Nimefikia uamuzi
huo kwa kuwa mpaka sasa ikiwa zimebaki siku chache Mkutano wa Tisa wa Bunge
kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 ambao Serikali iliahidi kuwa italeta marekebisho
ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii, mpaka sasa Serikali haijaitisha mkutano na
wafanyakazi pamoja na wadau wa jamii kupokea mapendekezo hali ambayo inaashiria
upo uwezekano muswada huo usiwasilishwe kwa wakati.
Lengo la Muswada
huo ni kufanya marekebisho yenye kuboresha mfumo wa utoaji wa mafao nchini
ikiwemo kuwezesha kutolewa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits) na mafao
mengine muhimu ambayo hayatolewi katika utaratibu wa sasa wa mifuko mbalimbali
ya hifadhi ya jamii.
Kwa upande mwingine
kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye marekebisho ya sheria
yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali ni udhaifu katika mfumo mzima wa
kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii nchini hali ambayo inahitaji wadau
kutaka mabadiliko makubwa.
Hapa akinukuu moja ya vipengele katika katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania |