Mawakili wa Kikundi cha Uamsho wakiongea na waandishi wa habari jana wakisoma Tamko la kutaka kujitoa katika kesi hiyo |
Mawakili wanaoshughulikia Kesi ya UAMSHO wametishia kujitoa katika kesi hyo kwa madai ya usumbufu wanaoupata wateja wao.
Mawakili hao ni Salim Tawfik na Abdallah Juma wanaowawakilisha Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake sita. jana wamesusa kabisa kuingia mahakamani na wamesema wanakusudia kujitoa kutokana na usumbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhawangaisha.
Mawakili hao jana waliondoka mahakamani na watuhumiwa walifikishwa mahakamani kutokea Mahabusu wakiwa wamenyolewa ndevu zote.
Watuhumiwa hao jana walisomewa Mashitaka mapya yanayowakabili miongoni mwa mashitaka ni kama yafuatayo.
1) Kusababisha uvinjifu wa amani zanziba
2) Kusababisha uharibifu wa mali kisiwani zanzibar kutokana na vurugu
3) Kushawishi na kuchochea vurugu zilizosababisha kuhatarisha maisha ya watu na serikali kuingia hasaraK
Aidha mtuhumiwa mmoja anatuhumiwa kumtukana Kamishna wa Polisi Zanzibar Musa Ally Musa
washtakiwa wote wamenyimwa dhamana kwani ni Jaji pekee ndie anayeweza kutoa dhamana kwa makosa yao lakini wana haki ya kukata rufaa kudai dhamana katika mahakama ya juu.
Sheikh Farid akionyesha alama ya vidole viwili akiwa amenyolewa ndevu wakati walipokuwa wanawasilishwa Mahakamani jana |