Habari ifuatayo imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Ziro99
Familia
ya walaghai wa Kiafrika imeiba kiasi kisichopungua Pauni za Uingereza
milioni 4 kutoka kwa walipakodi katika kipindi cha miaka 20.
Mmoja alitengeneza vitambulisho feki kwa watoto zaidi ya 100 ili kufaidi utaratibu wa mfumo wa mafao.
Pia
alidai kuwa na virusi vya ukimwi na kuhitaji dawa za gharama kubwa mno -
lakini badla yake alizisarifisha kinyemela kwenda nchini Uganda kwa
ajili ya kuziuza kwa faida kubwa.
Mahakama ilielezwa kwamba usafirishaji dawa hizo kwa miaka mingi uliwagharimu walipakodi zaidi ya Pauni za Uingereza milioni 2.
Zaidi
ya Pauni za Uingereza 154,000 zililipwa kwa ajili ya elimu kwa
'familia', ambapo Pauni za Uingereza 37,000 ni kwa ajili ya kozi moja tu
ya elimu ya juu.
Ulaghai unaohusiana na gharama za malazi na
kodi ya pango la maghorofa uligharimu Pauni za Uingereza 650,000, na
kiwango kikubwa cha mafao ya familia kinachofikia Pauni za Uingereza
900,000.
Kwa kipindi cha wiki sita cha usikilizwaji kesi yao,
baraza la mahakama lilielezwa jinsi kundi 'lililoungana kuandaa, kutumia
na kunyonya' utambulisho feki kwa lengo la kutekeleza ulaghai wa
kuduwaza.
Mchunguzi mmoja alilieleza gazeti la Daily Mail: "Balaa
ni, walikuwa na vitambulisho vingi mno kwamba inaweza isifahamike hasa
kiasi gani walichovuna kutoka kwenye mfumo wa mafao na nchi hii katika
kipindi hicho kirefu."
Mwendesha mashitaka Paul Raudnitz alisema:
"Mkono wa ulaghai huu umefika mbali na kwa mapana kwa miaka mingi sana.
Kila mshitakiwa kwa mara tofauti alishiriki njama hizo."
Alisema
'mshiriki mkuu' Ruth Nabuguzi mwenye miaka 49, 'ametumia vitambulisho
kadhaa ... vingi kiasi kwamba idadi ya vitambulisho haiwezi kufahamika'.
Nabuguzi,
mwenye asili ya kutoka Uganda, alidai dawa za Ukimwi zilizogharimu
Pauni za Uingereza 2,280,000. Pia alipokea Pauni za Uingereza 500,000
kwa ajili ya mafao ya nyumba kutoka Halmashauri ya Newham huko mashariki
mwa London, Mahakama ya Croydon ilielezwa.
Nabuguzi aliingia Uingereza mwaka 1991 na kuomba hifadhi ya ukimbizi yake mwenyewe na ya watoto wanne aliowaacha nchini Uganda.
Miaka
mitatu baadaye, alitumia jina la Jane Namusisi kuomba tena hifadhi ya
ukimbizi sambamba na ya watoto wawili zaidi. Mwaka 1999 akitumia jina la
Pauline Zalwango, aliomba tena hifadhi safari hii akiwa na watoto
wengine watatu.
Anaaminika amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda
Uganda na kuweza kununua nyumba takribani tatu ndani na maeneo
mbalimbali katika mji mkuu Kampala.
Dennis Kyeyune mwenye miaka
29, anadhaniwa kuwa ni mtoto wa Nabuguzi. Polisi walikuta begi jeusi
kubwa la kubebea nguo nyumbani kwake mashariki mwa London likiwa
limefichwa kwenye paa na mkoba wenye nyaraka bandia, ulioelezewa kama
'hifadhi ya ulaghai wa vitambulisho'.
Wafuasi wengine wa genge
hilo ni pamoja na Jordan Sebutemba mwenye miaka 26, ambaye anadhaniwa
kuwa ni binti wa Nabuguzi; Albert Kaidi, mshirika wa zamani wa Sebutemba
ambaye anadhaniwa kuwa na asili ya Rwanda; na Lamulah Sekiziyuvu mwenye
miaka 36, mshirika wa zamani wa Kyeyune na Kaidi.
Kyeyune, Sebutemba, Kaidi na Sekiziyuvu walipatikana na hatia ya makosa mbalimbali ya ulaghai juzi.
Watahukumiwa
wiki ijayo sambamba na Nabuguzi na Betty Tibakawa mwenye miaka 21, Lina
Katongola mwenye miaka 29, Mathy Matumba mwenye miaka 50, na Eddie
Carlos Semcenda mwenye miaka 30.