Wednesday, October 17, 2012

SHEIKH FARID WA UAMSHO ZANZIBAR NAYE ATEKWA NA MPAKA SASA HAJULIKANI ALIPO

Kwa habari nilizozipata hivi punde kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na Mitandao ni kwamba Huko Kisiwani  Unguja Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed  ametekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani yuko wapi.

 Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.
   Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
    Hata hivyo, wananchi wa hapa Zanzibar wanasema polisi, UAMSHO na serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao! Habari kupitia Mtandao wa Jamii forum