Tuesday, October 2, 2012

RUFAA YA LEMA YAGOMEWA BAADA YA KUIBUKA HOJA ZAIDI YA NANE


Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema akiwa nje ya mahakama baada ya rufaa yake kukataliwa




RUFAA  ya  aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema imeshindwa
kusikilizwa  baada ya  kuibuka kwa hoja zaidi ya nne ambazo zimewasilishwa na upande wa mawakili wa CCM  na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa hadi tarehe itakayopangwa  tena na
mahakama ya Rufaa.


Hoja hizo ziliibuliwa na  wakili wa ccm ,Alute Mughwai
akisaidiwa na wakili wa serikali Modest Akida wanaowawakilisha  wajibu rufani ambao ni
Agness Mollel, Happy Kivuyo na Musa Mkanga .

Hoja hizo zilianza kutolewa na  wakili wa wajibu rufani ,Mughwai kudai
kuwa rufaa iliyokatwa na Lema kupitia kwa mawakili wake, Method
Kimomogoro pamoja na Tundu Lissu imekosewa kwa kukiuka kanuni za
mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu pia katika rufaa hiyo hakuna mhuri
wa mahakama wala tarehe .

Alihoji ni kwanini Lema akimbilie kukata rufaa ndani ya siku 29 badala
ya siku 60 kwani hajapitia nakala ya hukumu ya awali hivyo endapo
angepitia hukumu hiyo pamoja na mawakili wake angeweza kujua
kunamatatizo gani na ayarekebishe badala yake wamekata rufaa bila
kuangalia kasoro zilizojitokeza.

Alisema ni lazima muhuri wa mahakama uwe pamoja na tarehe na kutokana
na umuhumi wa mhuri ndio maana hata mtu wa kijijini anaposhtakiwa au
kuhitaji msaada sehemu muhimu inabidi aende kwa mtendaji wa kijiji
kupata barua yenye mhuri na kuhoji ni kwanini Lema amekimbilia kukata
rufaa bila kuangalia kasoro zilizopo na kutoa rai kwa jopo la majaji
hao kutupilia mbali rufani hiyo ya Lema kwasababu haikakidhi matakwa
ya kisheria.

‘’Kwanini mmekimbili kukata rufaa bila kukagua kama kunakasoro katika
rufaa hii hivyo naomba jopo hili la majaji litupilie mbali rufaa hii
na Lema alipe fidia ya kesi hii,kwani kabla ya kukimbilia mahakamani
ni vema angehakiki nakala ya hukumu ndipo aje kufungua kesi na
kwatatizo hili naomba mahakama hii kutupilia mbali rufaa hii na Lema
ajipange upya’’.

Nao  Wakili wa Lema ,Kimomogolo alisema makosa yaliyotokea ni ya
kibinadamu na yamefanywa na mahakama na si Lema wala mawakili wao
hivyo aliwasihi majaji hao kutotupilia mbali rufani yao kwani katika
kesi kama hiyo ni lazima makosa madogo madogo yatokee na kusisitiza
mahakama kutenda haki kwa Lema.

Kimomogoro aliendelea kusema kuwa ikiwa wakili Mughwai alipewa ushindi
na mahakama kuu Kanda ya arusha hakupewa nakala ya hukumu iliyosahihi
je yeye aliyeshindwa angweza kuipata vipi nakala hiyo na kugundua
kasoro zilizopo na kuongeza kuwa mara baada ya hukumu jalada la kesi
hiyo lilipelekwa kwa Msajili wa  Mahakama ya Rufaa na pia walikuwa
wakipata taarifa nusunusu kutokana na kutokuwa na jadala hilo karibu
hivyo walishindwa kufuatilia .

Naye Wakili wa Serikali Timon Vitalis alisema anaounga mkoni hoja za
Kimomogoro za kutaka rufaa hiyo isikilizwe kwani tatizo lililojitokeza
kwenye hoja za wakili Mughwai si la Lema wala mawakili wake bali
tatizo ni la kimahakama hivyo mkata rufaa asiadhibiwe kwa kosa ambalo
si lao.

Alisema mahakama ndio inayopaswa kulalamikiwa katika kasoro
zilizojitokeza na si mkata rufaa na kuhusu hoja iliyotolewa na Mughwai
kuwa Lema achapwe fimbo kutokana na kasoro hizo aliongeza si sahihi
kwani mahakama si  sungusungu bali inasimamia na kutoa haki hivyo
aliwasihi majaji hao kuzipuuza pingamizi za kinaMughwai.

Naye Majaji ,salum Massati,Natalia Kimario  wakiongozwa na Jaji  Mkuu,
Mohammed Chande Othman  waliahirisha kesi hiyo hadi tarehe
itakayopangwa .

Baada ya kuahirisha kesi hiyo ,JAJI Mohammed Chande Othman alishukuru
wananchi waliojitokeza kusikiliza kesi mbalimbali katika mahakama ya
Rufaa na kuongeza kuwa mahakama hiyo ilianza usikilizwaji wa rufaa
mbalimbali Septemba 3 hadi Oktoba 2 mwaka huu.

Alisema katika kikao hiki wamesikiliza mashauri 36  na  katika vikao
vitatu vya mahakama ya rufaa wamesikiliza jumla ya mashauri 112 na
Arusha bado inamashauri mengi yakusikilizwa hivyo alidai kuwa
watajitahidi kupanga tarehe za mapema ili waweze kusikiliza mashauri
hayo na kuwashukuru polisi,magereza ,mawakili pamoja na wale wote
walioshiriki kufanikisha vikao hivyo.

Nje ya Mahakama ,umati wa watu uliokusanyika mahakamani hapo,
waliokuwa wameshika matawi ya miti walitawanyika kwa maandamano huku
wakipaza sauti ya People’s Power na kutaka uchaguzi urudiwe ili waweze
kupata mbunge katika Jimbo hilo.