Wednesday, October 3, 2012
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI KUHUSU KUDORORA KWA TTCL
Kwa mara nyingine tena najitokeza kuweza kutoa kero ambazo zina tupata Sisi Wananchi tunao tumia huduma za TTCL
Katika Mabadiliko ambayo Serikali ina himiza Wananchi katika kuingia katika Soko la Afrika Mashariki na ya Kati ni kujiendeleza kielimu lakini kuhizwa huko hakuko kwa TTCL wao bado na mfumo wa kizamani, Kwenye Umeme angalao serekari ime gundua kitu fulani kwa nini shirika hili naslo lisi chunguzwe kujua kama kuna masilahi ya watu au kukwama kwao kuna tokana na Elimu au ni watu wana kwamisha :?.
Watanzania tulio kuwepo katika Utawala wa Mwalimu Nyerere tuna usemi wa kusema usiache Mbachao kwa Msala upitao.
Methali hii inatubana kuitelekeza TTCL. katika Mitandao ambayo inaweza kumsaidia Mwananchi asiye na kipato ni TTCL lakini Shirika limekuwa na kiburi hata kama wateja wakilalamika Shirika la TTCL halisikii malalamiko ya wananchi .
Katika kutumia huduma za Internet .wateja wanalazimika kulipa kwenye mtandao wa TTCL Shilingi 30,000 kwa Mwezi au 7000 kwa Bando na hata Shilingi 500 ili waweze kupata huduma.
Cha kushangaza baada ya kulipa kwenye mtandao wa TTCL ili upate huduma unakuwa kama vile umepoteza fedha zako unaweza kuwa na kazi yhati inawezekana ika shindika kutuma yenye MB25 ukianza asubuhi ukiwa na bahati ita enda saa kumi jioni kama huna bahati ndiyo basi
Kama Una Attach file MB 25 unaweza kujanza Attachment Saa 2 Asubuhi ukafanikisha saa 9:00 Alasiri au ikakata.
Ukiingia kwen ye Mtandao mwingine Attachment hiyohiyo unachukua dakika 2 – mpaka dakika 5
Jee TTCL ina Wataalamu waliobobea ni vipi ishindwe kuweka Mazingira mazuri kwa wateja wao.
Wafanya kazi wa TTCL ambao hawakutaka Majina yao yatajwe wamedai wameweza kutoa Taarifa ya Malalamiko ya Wananchi hakuna kiongozi wa juu anaye tilia maanani malalamiko hayo.
Chamsingi kinachoonekana kwa TTCL badala ya kuboresha huduma wao wanawaza kuuza mali za TTCL kama walivyo fanya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ,
Mimi ni Mteja wa TTCL toka ilipo anza Namba yangu ya Simu 0252602425, Naishi Songea.
Ningeomba wa Tanzania kwa Wananchi wanategemea sana Mtandao wa TTCL, endapo hali ikiendelea namna hii basi Wale wote wanao ihujumu TTCL Serekari inge weza kuwa ajibisha. Haiwezekani Mitandao mingine ifanye kazi lakini mtandao wa Serekari Ushindwe kufanya kazi
By Adam Mzuza Nindi.-Songea