Wednesday, October 24, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI

Askari anayetuhumiwa kumuua mtangazaji w Channel Ten Daudi Mwangosi katikati aliyejifumika na sweater nyeupe akifikishwa mahakamani jana.

Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi jana alifikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili  huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.

Akisomewa shitaka lake na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian Ngilangwa, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mnamo Septemba mbili mwaka huu, huko katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, mtuhumiwa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya, Dyness Lyimo, mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Mtuhumiwa huyo aliletwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kaitka gari la polisi lenye number za usajili PT 1467. Waandishi wa habari wakizuiwa kupiga picha huku mwandishi wa gazeti la Majira, Elias Ally akisukumwa na mmoja wa Polisi hao.