Sunday, October 14, 2012

MGOMBEA NAFASI YA UJUMBE NEC AMTAKA RAIS AMN'GOE UANACHAMA WA CCM LOWASA,CHENGE BASHE NA WENZIE


Aliyekuwa Mgombea wa  Nec Taifa kupitia wilaya ya Bunda mkoani Mara Bw, Cyprian LM Musiba akizungumza na waandiishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam  juu ya Matakwa yake kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh Jakaya Mrisho Kikwete ambapo amemtaka Kuwanyang'anya uanachama wale wote wanao kihujumu chama hicho hatakama wanajitetea kuwa hawana Makosa yoyote awaondoe ili kukinusuru chama.
Musiba amesema kuwa wapo mafisadi wengi waliotajwa kuwa ni mafisadi lakini mpaka sasa bado ni wanachama wa CCM na wengine bado ni viongozi hivyo amemtaka Mwenyekiti wa CCM kuwan'goa katika chama kwa maslai ya kukilinda chama cha Mapinduzi.

Amewataja baadhi ya wanachama hao kuwa ni,Edward Lowasa, Hussei Bashe, Andrew Chenge,Vedasto Matayo,pamoja na Juliu Karanga na kusema kuwa hawa ni baadhi tu ya Wanachama wa CCM wanao kihujumu chama hicho kwa maslahi yao.
Bw, Cypria Musiba akizungumza na waandishi wa Habari waliohudhuria