Thursday, October 4, 2012

MASTERCARD KUPITIA ATM YA NBC YALIZA WATU

Wizi wa elektoniki unaonesha kushika kasi  jijini baada ya watu wawili kuibiwa fedha zao kwa kutumia MasterCard.

Mmoja wa waandishi waandamizi wa gazeti la HabariLEO, Bantulaki Bilango mwenye akaunti namba 017201056410 iliyofunguliwa katika tawi la NBC Moshi ameibiwa zote zilizokuwemo kwenye akaunti yake kupitia ATM ya tawi la Benki hiyo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutoa taarifa NBC Makao Makuu yaliyopo Mtaa wa Sokoine Drive mapema leo, Bilango alisema baada ya kutoa fedha katika akaunti yake kupitia ATM iliyopo tawi la benki hiyo la Viwandani barabara ya Nyerere jana, leo alikupokwenda ATM zilizopo katika tawi la Corperate, alikuta fedha hizo zimechukuliwa muda mfupi kabla yake.

Taarifa ya benki aliyopewa ilionesha kuwa pesa hizo zilitolewa leo asubuhi katika ATM iliyopo Kinondoni.

Scan sehemu ya statement uonyeshe jinsi gani mwizi huyo alivyoiba.

“Jamani huu wizi ni wa aina yake. Mimi nimechuka Master Card yangu juzi tu leo hii kuna mtu amekomba pesa zangu zote kwenye ATM,” alisema .

Hata hivyo alipoomba waangalie kamera zao kwa kuwa kila anayeingia kwenye mashine za ATM humulikwa walidai kuwa hiyo ni hatua ya juu sana inayohusisha polisi, hivyo hawawezi kufanya hivyo kwa wakati ule.

Hata hivyo, Bilango anasema alipata ushirikiano mzuri katika tawi la benki ya Viwandani katika barabara Nyerere alikochukulia fedha jana ambapo msimamizi wa Huduma kwa Wateja na Huduma za Biashara na Nje, Matilda Manumbu kwa kushirikiana na viongozi wengine wa benki hiyi waliahidi kufuatilia kwa karibu ili kuweza kumpata mhusika.

Kulingana na maelezo ya Bilango, kadi iliyokuwa ikitumika kuiba fedha ni ile ile ambayo alikuwa anayo mfukoni. Alisema la kushangaza, wakati yeye akiwa nayo, mtu mwingine alikuwa akiendelea kutoa fedha katika ATM.

Mmoja wa wateja alisema wizi huo unaoweza kufanyika kwa kuwatumia wafanyakazi wa benki lakini wakati mwingine kuna carbon inaachwa kwenye mashine ya ATM ambapo mteja akiweka kadi, taarifa zake zinanaswa kwenye carbon hiyo na baada mwizi kutumia taarifa hizo kuiba fedha hizo katika ATM nyingine.

Alishauri wateja kuacha kutumia njia hiyo na badala yake watumie dirisha kwa kuwa mashine hizo zinatumiwa vibaya.

Wizi huo unaonekana kukithiri hasa katika tawi la Kinondoni ambapo mteja mwingine ambaye hakupenda kutaja jina lake alichukulia fedha zake katika tawi hilo la Viwandani, kisha kuibiwa fedha zake kupitia tawi la Kinondoni wiki iliyopita kwa kutumia kadi yake ya ATM .

“Nami nimelizwa, lakini wamesema wanashughulikia, hivyo naamini fedha zangu zitarudishwa maana walichukua mshahara wangu wote.

Tukio hilo lilimpata tena mkazi mwingine, Fabian Rugaimukamu mwenye akaunti namba 2012401429 katika benki ya NMB tawi la Bank House.

Source: .wavuti.com-wavuti