Nayo Ruvu Shooting itaikaribisha
Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa
Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
Jumapili (Oktoba 7
mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT itakayochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini
Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya).