Hii ni gari inayobeba mahabusu |
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo,limetokea majira ya saa 7.30 mchana katika mahakama kuu jijini
Arusha ambapo tukio hilo lilizua hofu kubwa mahakamani hapo baada ya
kuwalazimu baadhi ya watumishi wa mahakama hiyo kujifungia ndani ya
vyumba vya mahakama wakihofia mahabusu huyo kuwafyatulia risasi.
Taarifa zimedai kwamba mahabusu
huyo alikuwa wa kwanza kutoka kwenye chumba cha mahabusu na
alipomkaribia askari huyo ambaye pia hajafahamika ghafla alivaa na
kumpora silaha hiyo inayodaiwa kuwa na risasi 30 na kuruka uzio mrefu wa
mahakama hiyo.
Mashuhuda walisema kuwa mahabusu
huyo wa jinsia ya kiume alitokomea na silaha hiyo kwenye mto sanawari
uliopo pembezoni mwa mahakama hiyo, hata hivyo baadae aliitelekeza
silaha hiyo na polisi walifanikiwa kuipata .
‘’unajua tukio hilo limewshtua
watu sana hawawatumishi wa mahakama walijifungia ndani wakihofia usalama
wao hata hawa watu wanaokaahapa kusikiliza kesi za ndugu zao wote
walitawanyika ‘’alisema shuhuda huyo n akuongeza kuwa
‘’si jambo la kawaida kutokea
ila kuna uzembe Fulani umefanywa na polisi kwani haiwezekeni askari
aporwe silaha tene smg akiwa ameishikilia ,hii ni hatari sana ‘’
Baada ya tukio hilo polisi
walianza kuhaha kumsaka mahabusu hiyo na kwamba wakati wakipita eneo
alilokimbilia walifanikiwa kuikuta bunduki hiyo ikiwa imetelekeza kwenye
mawe ene la mtoni.Hata hivyo haikufahamika mara moja mahabusu huyo alikuwa akikabiliwa na makosa gani mahakamani hapo .
Kamanda wa polisi mkoani Arusha
Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba
polisi inafanya uchunguzi wa tukio hilo huku wakifanya msako mkali wa
mahabusu hiyo.
Reported byMahmoud Ahmad via:Full shangwe