Monday, October 8, 2012

BARABARA YA KIMARA-KING'ONG'O YAKERA,MKURUGENZI MANISPAA YA KINONDONI APEWA SIKU 7 TU.

DIWANI wa Kata ya Saranga (Chadema), wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kutekeleza makubaliano ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kimara hadi King’ongo kinyume chake wakazi wa eneo hilo wataandamana.
Kauli hiyo imekuja baada ya wakazi hao kuhoji kuhusu sh milioni 300 zilizotolewa na wafadhili wa Japan, Mei mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 3.8, haujaanza hadi leo wakati fedha zipo. 
Akizungumza na wandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, diwani huyo, Efraim Kinyafu, alisema wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakitaabika kwa muda mrefu kutokana na ubovu wa barabara hiyo kitendo kwamisha shughu zao za maendeleo.
Alisema wameamua kutumia utaratibu huo wa kuandamana kama njia sahihi ya kufikisha kilio chao kwa wafadhili waliojitolea fedha hizo, hata hivyo, itategemea iwapo siku saba zitapita bila ya mkandarasi kuwepo katika maeneo hayo
Kinyafu alisema wafadhili hao walipinga fedha hizo kupitia kwenye Akauti ya Manispaa ambapo  walikubaliana zipitie kwenye Akauti ya kata.
Akifafanua zaidi, alisema baada ya makubaliano hayo ofisi ya kata iliwasilisha Akaunti yake kwa Mkurugezi kisha utekelezaji wauingizaji wa fedha hizo ulikamilika tangu Mei mwaka huu.
“Unajua wananchi hawaelewi kuna nini kinaendelea  wakati kuna jumla y sh milioni 350 amapo kati ya hizo halmashauri imechangia milioni 50 isitoshe hata kapuni ya ujenzi ya COSCO imeishapewa tenda ya kazi hiyo”alisema kinyafu.
Kinyafu alitoa angalizo kwa viongozi wa Manispaa hiyo kuepuka mgogoro huo kwani unaweza ukawa mkubwa zaidi kushinda ule ulijitokeza wakati wa sensa ya makazi na watu kutokana na ukweli kwamba waathirika safari hii ni wengi.
Alisema mvutano huo wa ucheleweshwaji wa miradi mingi katika maeneo yanayoongozwa na vyama vya upinzani kunachangiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakidhani kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kwa asilimia 100 kutawajengea umaaruf wapinzani hao, kuwafanya waendelee kuchaguliwa katika chaguzi nyingne kitendo ambacho hakina uhakika.