Monday, October 22, 2012

KESI YA LULU YA AHIRISHWA TENA

Msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael a.k.a LULU, (Katikati), akielekea kupanfa basi la magereza kwenye viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, baada ya kesi inayomkabili ya kutuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Hayati Steven Kanumba, kuahirishwa tena na hivyo mwanadada huyo ambaye umri wake unaleta utata ataendelea kusota rumande hadi hapo kesi yake itakapotajwa tena. (picha via K-VIS)

MSANII  wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, amehoji Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu lilikofikia jalada la kesi.

Lulu aliuliza swali hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Stuarti Sanga baada ya Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi wake haujakamilika.

Baada ya Sekwao kueleza hiyo, Lulu alinyoosha mkono na kuhoji jalada la kesi inayomkabili lilikofikia. Hakimu Sanga alimuuliza Wakili Sekwao iwapo anauliza jalada halisi au la kudurufu.

Wakili Sekwao alimwambia Hakimu Sanga kuwa, anaulizia jalada halisi.Hakimu Sanga alimwambia Lulu kuwa jalada halisi limekwisharudi  na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu itakapotajwa tena.

Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwa Kanumba, Sinza, Dar es Salaam.

Habari imeandikwa na Tausi Ally via MWANANCHI



Lulu akiwapungia Mashabiki wake wakati akielekea kupanda ari la Magereza