Kuna
taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za
simu kwamba kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na
kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa
waangalifu.
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Tunapenda kutoa taarifa
kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake haliwezi kuwa zuri kwa
Watanzania. Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba
hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.
Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.