Watu wanne wanasadikiwa
kupoteza maisha usiku huu October 21 2012 baada ya kutokea fujo Karatu
kwenye Pub maarufu iitwayo Pub Lamonte.
Kwa wiki kadhaa matangazo
yamekua yakisikika na mabango kuonekana ikitangazwa kwamba Mwimbaji
BARNABA atakua na show Pub Lamonte Karatu usiku wa october 21 2012
ambapo watu walinunua ticket na wakajaa kwa ajili ya kumsubiria Barnaba.
Kilichotokea ni kwamba kumbe
Promota hakuwahi hata kuongea na Barnaba ambae ndio ameingia Dar es
salaam akitokea Nairobi leo, sasa leo ikiwa ndio siku ya show Promota
kampeleka Barnaba feki ambae nimeambiwa ni mrefu na amejazia ambapo
hakuchukua time watu kumgundua kwamba ni feki, fujo ndio zikaanza kwa
watu wenye hasira na viingilio walivyolipa.
Mabaunsa wamepambana lakini
taarifa nilizozipata ni kwamba visu na chupa zimetumika kama silaha,
naendelea kuifatilia zaidi hii habari hivyo endelea kuwa karibu na
millardayo.com pamoja na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kwa taarifa zaidi.
Source: Millard Ayo |