Sunday, October 21, 2012

MASHINDANO YA 2020 WORLD SQUASH DAY YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mashindano ya Squash 2020 yamefanyika juzi Katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ambapo timu m balimbali nchini Tanzania Zilishiriki katika mashindano hayo.Mgeni rasmi katika Mashindano hayo alikuwa ni Rais wa Kamati ya Olympiki nchini Bw, Rashid Gulam ambaye alisema kuwa anawashukuru waandaaji wa mashindano hayo kwa kuonyesha kuwa mashindano hayo yapo na kuahidi kuwa wao kama Olymppiki watatoa Ushirikiano katika mchezo huo wa Squash.

Wachezaji wakiwa Uwanjani katika mashindano hayo

Mwandishi wa habari wa Channel ten akiripoti mchezo huo katika viwanja vya Gymkhana

Baadhi ya matokeo ya Mchezo huo baada ya Mchezo kumalizika


Mwenyekiti wa Squash akisema jambo la Shukrani kwa washiriki wa Mchezo huo


Baadhi ya wanamichezo wakisikiliza kwa makini

Waandishi wa habari wa Magazeti pia walikuwepo, Kushoto ni Joseph Mchekadona wa Gazeti la The Guardian na lasteck Mushi wa Gazeti la Citizen wakifwatilia mchezo huo kwa Makini