Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Mhe. Dkt.
Getrude Rwakatare ametoa Ujumbe kwa Watanzania waliohudhiria Ibada
Maalum ya Kuliombea Taifa ambapo ametaka watu kutobaguana kwa misingi ya
Dini, Ukabila wala Siasa na kusema pamoja na Utawala Bora pia
tunahitaji maombezi ili tuweze kufikia malengo yaliyokusudiwa kulipeleka
Taifa linapotakiwa kufikia.
Dkt. Rwakatare amesema nia kubwa ya
kufanya Ibada hiyo ya Maombezi ni kutaka kuweka usawa kutokana na siku
za hivi karibuni kuibuka kwa matamko mbalimbali kutoka kwa watu tofauti
wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini na wa baadhi ya makundi
yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la Mungu kila kitu
kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani
na Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni kimbilio la watu wa
Mataifa mbalimbali.
Akasema Watanzania hawajui kuchukiana na wamekuwa watu wa kushikamana kwa miaka yote.
|