Ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyopata ajali jana asubuhi katika Kambi ya Jeshi la Anga (Air wing) Ukonga jijini Dar es Salaam baada ya kushindwa kuruka. (Picha kwa hisani ya JWTZ) |
Akielezea juu ya ajali hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kanali Kapambala Mgawe, alitaja jina la aliyepoteza maisha kuwa ni Kapteni Mangushi na aliyejeruhiwa kuwa ni Kampeni Kilikila.
Anasema kuwa wanajeshi hao wanafunzi walikuwa kwenye mafunzo ya kawaida, ambapo waliipanda ndege hiyo ya kivita huku wakiwa na miavuli, na baada ya kuruhusiwa walifyatua kitufe cha kupaa ndege, lakini bahati mbaya ilishindwa kwenda angani na paa lake kugonga hanga la kutengenezea ndege. Ndege hiyo ilitakiwa iruke kama risasi umbali wa mita 100 kwenda angani.
Anasema ndipo wanajeshi hao waliokuwa wamevaa miavuli walitupwa nje, ambapo mmoja aliyejeruhiwa aliangukia kwenye lami barabarani na aliyekufa alijigonga juu ya paa la hanga baada ya mwavuli aliokuwa nao kushindwa kufunguka.
Mgawe anasema kuwa kawaida tahadhari zinakuwepo, ila kwa tukio hilo bado hawajatambua tatizo lilikuwa ni nini.
Anasikitika kumpoteza mmoja wa wanajeshi wapiganaji hao.