KATIBU Mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi
amefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki mkutano mkuu wa Taifa wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) akiwakilisha Wilaya ya Karatu.
Bayi
amefanikiwa kukata tiketi hiyo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi
karibuni baada ya kupata kura 264, ambapo ataungana na Mary Sulley(545),
Ori Pembe (460), Fabiola Deo (456) na Amsi aliyepata kura 322.
Katika
uchaguzi huo, nafasi ya uenyekiti ilikwenda kwa Mustafa Mbwambo
aliyepata kura 512 na hivyo kumwangusha Gerald Gwaha aliyepata kura
148 huku mgombea mwingine aliyefahamika kwa jina la Tippe alijitoa
katika kinyang’anyiro hicho.
Kwa upande wa nafasi
kamati kuu ya halmashauri kuu (NEC), Awaki Tlemai alishika nafasi ya
kwanza kwa kupata kura 545 na Daniel Ilakwahhi aliyekuwa wa pili kwa
kupata kura 114.