Saturday, October 6, 2012

FIESTA YAFANA DAR ,NI BAADA YA RICK ROSS KUTINGA JUKWAANI


Rick Ross akiwaelekeza mashabiki jambo alipokuwa jukwaan

Rick Ross akiwapagawisha mashabiki wake

Watu wa usalama wakiimarisha amani

Lina akionyesha mambo yake akiwa jukwaani

Rachel Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na  wacheza shoo wake  katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kuu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo kali usiku huu.
Mwanamuziki Diana wa muziki wa Bongofleva kutoka kundi la THT akiimba katika Tamasha hilo
 






Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephraim Mafuru na kutoka kushoto Meneja wa Masoko SBL Emmilian Rwejuna na Mdau Rawlence Mafuru pamoja na wadau wengine wakipozi kwa picha.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw Ephraim Mafuru akitangaza mshindi wa bahati nasibu ya magari mawili kwa mkoa wa Dar es salaam iliyoendeshwa katika matamasha yote ya Serengeti Fiesta mwaka huu kutoka kulia ni Bw. Mrisho kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha , Rugambo Rodney Meneja masoko wa Push Mobile na kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Entarteinment Bw Joseph Kusaga wakishuhudia tukio hilo

Mashabiki wakipagawa baada ya Rick kutinga jukwaani