TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WASAFIRI WETU WA RELI YA KATI DARAJA LA TATU
KWAMBA, KUANZIA SASA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA SABA WATASAFIRI BURE
NA WATAPEWA KITI/VITI.
WATOTO HAO WATATAKIWA KUSAFIRI NA
WAZAZI/WALEZI WAO NA PIA WAJE NA VYETI VYA KUZALIWA AU BARUA YA SERIKALI
YA MTAA HUSIKA KUTHIBITISHA UHUSIANO NA MZAZI/MLEZI WAKE.
MZAZI/MLEZI
ATAKAYESAFIRI NA WATOTO HAO ATARUHUSIWA WATOTO WASIOZIDI WAWILI KWA
WAKATI MMOJA NA NILAZIMA AJE NA VITHIBITISHO HIVYO WAKATI WA KUNUNUA
TIKETI YAKE NA AWAANDIKISHE KWA KARANI/STESHENI MASTA ILI WAWEZE KUPATA
TIKETI ZA KUSAFIRIA.
MTOTO ATAKAYEKUTWA NDANI YA TRENI BILA
TIKETI ATALIPIA NUSU NAULI YA MTU MZIMA. TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI
KUBORESHA HUDUMA HII.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TRL Mtendaji Mhandisi Kipallo A.Kisamfu Dar es Salaam.