Wednesday, October 3, 2012

MHE.MWANJELWA NA DEREVA WAKE WAHAMISHIWA DAR KWA MATIBABU ZAIDI


Dkt. Mwanjelwa akiwa hospitalini Ifisi asubuhi ya leo. (picha: Mkwinda)


Imeelezwa kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Viti Maalum CCM, Dkt. Mary Mwanjelwa anasafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya huduma zaidi za kiafya baada ya kunurusika ajalini jana.

Dkt. Mwanjelwa alikuwa amelazwa katika hospitali teule ya Ifisi tangu jana.

Ameweza kuzungumza kwa ufasaha na kuwatambua watu aliokuwa wanaingia na kutoka kumjulia hali.

Alisema, "Hali yangu ni nzuri, najisikia maumivu sehemu za kiunoni na kwenye mbavu, lakini najisikia vizuri".

Nje ya wodi alimokuwa amelazwa walikuwepo baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na wananchi waliokwenda kumjulia hali.