Friday, September 21, 2012

TUME YA USHINDANI WASAINI MKATABA NA MICROSOFT NI WA KUPAMBANA NA MAHARAMIA WANAOHUJUMU PROGRAMU ZA COMPYUTA

Mkurugenzi  Mkuu wa Microsoft Africa ya Mashariki na kusini Bw Erick Odipo akisaini Mkataba huo ambapoa amesema kuwa  mkataba huu utahakikisha kuwa bidhaa bandia za programu za  Compyuta  nchini  zinakomeshwa ambapo itasaidia kukuza ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Aidha Bw, Odimpo amesema kuwa   mashirika hayo mawili yaliyosaini mkataba huo  wataendeleza kwa pamoja program na Kampeni  za kuelimisha na kutoa taarifa  kwa wakala na Umma  kuhusu hatari  na adhabu zinazo husishwa na ukiukwaji wa haki miliki ya program na ukiukwaji alama ya biashara yaani trade mark.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani Tanzania  Bw, Allan Mlula akisaini mkataba  wa kupambana na vitendo  vya  kihalifu vya kutengeneza bidhaa za  Microsoft ambazo siyo halisi. Mkataba huo umesainiwa na Tume ya Ushindani pamoja  na Microsoft ambapo kwa pamoja watashirikiana kupambana na uhalifu huo ambao amesema kuwa umekithiri sana nchini Tanzania.

Mkurugenzi  Mkuu wa Microsoft Africa ya Mashariki na kusini Bw Erick Odipo akionyesha baadhi ya CD za program bandia za Compyuta.

Mfano wa programu feki ya compyuta

Baadhi ya wadau walioshiriki katika Mkutano huo

Waandishi nao walikuwepo