Waandamanaji wakiwa wamefunga barabara eneo la kwa Ngulelo (Arusha-Moshi) kwa kutumia mawe na wote ni Madereva wa Pikipiki maarufu kama BodaBoda |
Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara hiyo kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .
Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki, Jonathan Emanuel, Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru, maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36) mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Septemba 15 mwaka huu akiwa barabarani eneo la Baraa akimsafirisha abiria aliyekuwa amemkodi.
Madereva hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia mtuhumiwa wa mauaji (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na mmiliki wa garage ya kutengeneza magari na mkazi wa Baraa, walilituhumu jeshi la polisi mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.
Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali za mtuhumiwa ikiwemo gari lake lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya nyumba hiyo.
Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kufika eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.
Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva hao walivunja vioo vya magari kwa kupiga mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.
Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwao eneo la Oldadai
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana mara moja jina lake akitaka kupasua kioo cha gari dogo baada ya dereva wa kagi hilo kutaka kupita eneo walilosuia. |