Saturday, September 29, 2012

SUPERSPOT YAITANGAZA TANZANIA MICHEZONI KIMATAIFA

Mkuu wa Super Sport barani Afrika Bw. Andre Venter akielezea furaha yake kuja Tanzania na kupata fursa ya kulitangaza soka la Tanzania kimataifa kupitia chaneli ya Super Sport amesema chaneli hiyo imechafanya kazi katika nchi za Kenya na Uganda na Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha kiwango chake cha soka Kimataifa.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Leordgar Tenga akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Soka Tanzania ambapo amevitaka vilabu vitakavyopata bahati ya kuonekana katika chaneli hiyo kuonyesha kiwango cha soka la Tanzania na kuzingatia nidhamu haswa mechi ya Watani wa Jadi Yanga na Simba ambao wanatambulika barani Afrika kama timu zenye upinzani mkali.


Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo kuwa Super Sport wakishirikiana na TFF wapo hapa nchini na kwa mara ya kwanza wanaonyesha mechi za Ligi ikiwemo timu ambazo hata siku moja hazijawahi kuonekana kwenye Chaneli ya Super Sport na kuwataka wachezaji wa timu hizo kuonyesha uwezo wao kwa sababu ni fursa ya pekee kuonekana katika nyanja ya Kimataifa. Aidha amewataka Watanzania ambao hawajaunganishwa na DStv wafanye hima kununua ving'amuzi ili waweze kushuhudia mechi hizo pamoja na chaneli nyinginezo zinazopatikana katika DStv.