Saturday, September 29, 2012

MACHINGA COMPLEX SASA KUWA SOKO LA KISASA: NI BAADA YA KUPIGWA TAFU NA EQUTY BANK PAMOJA NA AIRTEL

Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Gulio expo20 wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yanaendelea


Mwenyekti wa Bodi ya Machinga Complex Bw, Godwin Mbaga akizungumza katika mkutano wa kuzindua progaramu ya Gulio Expo 20 ambao itafanya kazi kwa wa siku 20 za Matangazo, Burudani pamoja na kuuza na kununua bidhaa katika Soko la Machinga Complex , utakaoanza siku za karibuni mwezi ujao  yenye nia ya kulitangaza Jengo la Machinga complex.
Programu hiyo ya Gulio expo imedhaminiwa na makampuni mengi yakiwemo Benki ya Equity pamoja na Airtel ambapo  Wafanyabihashara wa Machinga complex wataweza kukopa kwa gharama nafuu kuanzia 100,000 hadi 5000,000 na wataweza kulipa kupitia account ya airtel money.

Huyu ndo mwenyekiti wa Bodi


Mkurugenzi wa Ear Promotion inayojishughulisha na Gulio Expo 20, Bw,Brian Kikoti, akisoma Risala katika uzinduzi huo wa mpango wa kulitangaza jingo la Machinga complex ambapo katika risala yake amesema kuwa  kampuni yake ni muungano wa kampuni zilizo amua kuunganisha nguvu ili kufanya kazi pamoja  kwa lengo la kukuza  bihashara zenye Weledi wa bihashara na masoko pamoja na uandaaji wa matamasha na Matangazo.
Amesema kuwa kampuni yake imeweza kusajili wafanyabihashara 500 ambao wanavitambulisho vya kisasa kabisa.


Mwenyekiti wa Machinga Complex Bw, Abubakary Rakesh akitoa shukurani zake kwa wadhamini wa waliojitokeza kuliinua soko hilo, ambapo amesema kuwa kuanzia sasa soko la machinga Complex litakuwa na bidhaa nzuri na kwa gharama nafuu.

Wafanya Bihashara waliokuwemo katika Hafla hiyo wakisikiliza kwa makini