Friday, September 28, 2012

RAPA RICK ROSS KUTUA BONGO FIESTA

Na Semvua Msangi
Ni wazi kuwa joto la wapenda burudani kwa sasa litakuwa limepanda hadi degree 43 zaidi ya lile la jiji la Khartoum kutokana na kusubiri kupewa taarifa ya msanii gani wa kimataifa atakayekuja kuwasha moto wenye jukwaa la Fiesta 2012 BHAAAAAAAAS.

Kabla ya wahusika kutangaza ni nani anayekuja team BaabKUBWA Magazine we have the name of who’s coming for us!! Guess whaaaat……. Mayback Music Group president call him Rick Ross, Rozay aka The BOSS all tha way from US of America ndiye anayekuja kuonyesha U-boss wake jijini.

Taarifa za awali zilikuwa zikidai kuwa Rozay alikuwa akafanye show jijini Nairobi Ijumaa ya tarehe 5 October mwaka huu ambayo kesho yake ndiyo siku ya Fiesta jijini lakini ma-promoter wa nchi hiyo wameshindwana nae.

Mara ya mwisho alipokwenda kufanya show South Afrika, Wakenya waliambulia kumwona Rozay kwenye uwanja wao wa ndege wa Jomo Kenyata International Airport{JKIA}.

This time around Rozay atapita tena Kenya akija Tanzania kuja kufanya the so called an electrifying, unforgettable, big time performance in Tanzania kwenye Serengeti Fiesta 2012 BHAAAAAAS itakayofanyika kwenye viwanja vya Leaders hapa jijini Dar es Salaam tarehe 6 October 2012.