Ndugu na majirani wa Neema John wakijitahidi kumpepea Neema
akiwa ndani ya gari kusubiri fomu ya Polisi
katika kituo cha polisi buguruni baada ya kumwagiwa mafuta ya moto
mwilini na Dada yake Monica John katika ugomvi wa kugombania kiporo cha ubwabwa
leo asubuhi.
Kwa mujibu wa mashuhuda tafrani hiyo ilitokea leo asubuhi
katika eneo la Tabata kisiwani kwa kipingu baada ya Monica kudai kiporo cha
wali kilichobaki jana ili aweze kukitumia kama kidfungua kinywa ambapo
alielezwa na nduguye kuwa ameshakila ndipo ugomvi ukaanza na kufikia kumwagiana
mafuta.
Kufuatia tukio hilo Monica alikamatwa na askari
wa jeshi la Polisi wa kituo cha Polisi Tabata kisiwani na kufikishwa buguruni
kwa hatua zaidi ambapo ndugu yake amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala |