Wednesday, September 26, 2012

NAMNA UFUGAJI UNAVYOWEZA KUMFAIDISHA MTU


Nimevutiwa sana na maelezo ya Ng'wanambiti, Chacha o'Wambura kwenye blogu yake alipoandika, “Japo ni kijijini, bado twaweza kufuga kisasa!” kwa kuwa imenipa somo zuri sana kuhusu ufugaji na utunzaji wa kuku na mayai yake vizuri.

Chacha anasema,

Ni ndani ya shamba ambalo kiukweli ni msitu wa ukweli ambao ni takribani kilomita za mraba 50 na humo anaishi mwenye shamba Bw. Aidan Paulus Kenyero katika kijiji cha Liganga, wilaya ya Mbinga.

Bwana huyu pamoja na kujihusisha na kilimo cha mazao lakini pia anafuga mifugo…ngómbe zaidi ya 70 na vitu vingine. Nimejifunza namna ya kuhudumia kuku wa mayai na kuepusha mayai kuvunjika pindi yakishatagwa.

Bwana huyu ana nyumba ya ghorofa moja ilojengwa humo msituni mwaka 1989 na anatumia umeme wa gesi (Biogas) ambapo ana mitambo 2. Anacho pia kiwanda cha sukari lakini hakifanyi kazi kutokana na ukiritimba wa serikali hivo amekifunga na mitambo ipo tu imelala.


Kuku akishataga mayai yanashuka yenyewe na kudondokea hapa anapoonyesha

Haya ndio mayai yaliyotagwa

Mafanikio ya bwana Aidan haya ni magorofa yake.