Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa
gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo umeagwa leo mchana
Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya mazishi kesho mjini
Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New Habari 2006 Limited, alifariki
dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa
amelazwa kwa matibabu.
Katika uagwaji wa mwili wa marehemu,
aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi, mamia walijitokeza na wengi
walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi kupoteza fahamu. Hakika
ilikuwa huzuni, simanzi na majonzi eneo la tukio. Agness ameliza watu.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu, Amin. |