Wednesday, September 26, 2012

JK, ASHIRIKI KUMUAGA ALIYEKUWA MKURUGENZA WA KWANZA WA TAKUKURU

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali Mstaafu  Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati  Meja Jenerali Mstaafu  Anatoli Kamazima,  leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam.  Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.