Wednesday, September 26, 2012

UFAFANUZI KUHUSU MATUMIZI YA VOCHA YA 450 YA VODA


Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imekuwa na taarifa na malalamiko mbalimbali kuhusiana na mauzo ya vocha ya Shilingi 450/- inayouzwa  kwa bei ya juu Tsh. 500/- wakati vocha hizo kiuhalali zinauzwa kwa Tsh 450/-.

Vocha hizi za TSh. 450/- zimetolewa katika soko ili kuwawezesha  wateja wetu kuwa na mawasiliano ya urahisi zaidi.

Bei halali ya vocha hii ni TSh. 450/- kama ilivyo andikwa kwenye Vocha na tunawahimiza wateja wetu wanunue vocha hizo kwa bei halali  iliyotangazwa, na siyo vinginevyo.

Tunashukuru kwa maoni yenu juu ya hili swala na tunafatilia kwa ukaribu zaidi kwa wauzaji wa vocha hizi kuhakikisha wanatoa huduma bora na ya uhakika kwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla.

Tafadhali, shirikiana nasi kwa kutoa taarifa mbalimbali hususani kuhusina na swala hili la vocha hizi za TSh. 450/- kupitia kurasa zetu za Facebook na Twitter.